Asia ni bara kubwa kabisa kuliko mabara yote mengine ya dunia. Bara hili lina eneo la kilomita za mraba 44,579,000 (maili za mraba 17,212,000), ambalo ni sawa na asilimia 30% ya ardhi yote. Wakazi wa bara la Asia ni 3,701,000,000 kwa mujibu wa makisio 2003.

Asia

Bara la Asia lina nchi 44 na visiwa mbali mbali vya madola mbalimbali. Mlima mrefu kabisa ulimwenguni ambao ni mlima wa Everesti wenye urefu wa mita 8,850 (futi 29,035) ulioko Nepal pia uko kwenye bara hili. Kadhalika, nchi zenye wakazi wengi zaidi ulimwenguni China na India pia ziko kwenye bara hili.

Ziwa kubwa kabisa ulimwenguni, bahari ya Kazwini (Caspian Sea) lenye eneo la kilomita za mraba 394,299 (maili za mraba 152,239) vile vile liko Asia kati ya ya nchi hizi: Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan, na Uajemi.

Bara la Asia linaweza kugawanywa katika sehemu zifuatazo:

Orodha ya nchi na maeneo hariri

     Asia ya Kaskazini      Asia ya Kati      Asia ya Magharibi      Asia ya Kusini      Asia ya Mashariki      Asia ya Kusini-Mashariki
Jina la nchi au eneo,
bendera
Eneo
(km²)
Wakazi
(1 Julai 2008)
Wakazi kwa km²Mji mkuu
Asia ya Kati:
Kazakhstan
2,724,92715,666,5335.7Astana
Kirgizia
198,5005,356,86924.3Bishkek
Tajikistan
143,1007,211,88447.0Dushanbe
Turkmenistan
488,1005,179,5739.6Ashgabat
Uzbekistan
447,40028,268,44157.1Tashkent
Asia ya Mashariki:
Uchina
9,584,4921,322,044,605134.0Beijing
Hong Kong
1,0927,903,3346,688.0
Macau
25460,82318,473.3
Japani
377,835127,288,628336.1Tokyo
Taiwan
35,98022,920,946626.7Taipei
Korea Kaskazini
120,54023,479,095184.4Pyongyang
Korea Kusini
98,48049,232,844490.7Seoul
Mongolia
1,565,0002,996,0821.7Ulaanbaatar
Asia ya Kaskazini:
Urusi
17,075,400142,200,00026.8Moscow
Asia ya Kusini-Mashariki:
Brunei
5,770381,37166.1Bandar Seri Begawan
Myanmar
676,57847,758,22470.3Pyinmana
Kamboja
181,03513,388,91074Phnom Penh
Timor Mashariki
15,0071,108,77773.8Dili
Indonesia
1,919,440230,512,000120.1Jakarta
Laos
236,8006,677,53428.2Vientiane
Malaysia
329,84727,780,00084.2Kuala Lumpur
Ufilipino
300,00092,681,453308.9Manila
Singapuri
7044,608,1676,545.7Singapuri
Uthai
514,00065,493,298127.4Bangkok
Vietnam
331,69086,116,559259.6Hanoi
Asia ya Kusini:
Afghanistan
647,50032,738,77542.9Kabul
Bangla Desh
147,570153,546,9011040.5Dhaka
Bhutan
38,394682,32117.8Thimphu
Uhindi
3,287,2631,147,995,226349.2New Delhi
Uajemi
1,648,19570,472,84642.8Tehran
Maledivi
300379,1741,263.3Malé
Nepal
147,18129,519,114200.5Kathmandu
Pakistan
803,940167,762,049208.7Islamabad
Sri Lanka
65,61021,128,773322.0Sri Jayawardenapura
Asia ya Magharibi:
Armenia
29,8002,968,586111.7Yerevan
Azerbaijan
46,8703,845,12782.0Baku
Bahrain
665718,306987.1Manama
Kupro
9,250792,60483.9Nikosia
Palestina
3631,537,2693,315.7Gaza
Georgia
20,4604,630,84199.3Tbilisi
Irak
437,07228,221,18154.9Baghdad
Israel
20,7707,112,359290.3Yerusalemu
Yordani
92,3006,198,67757.5Amman
Kuwait
17,8202,596,561118.5Jiji la Kuwait
Libanon
10,4523,971,941353.6Beirut
Omani
212,4603,311,64012.8Muskat
Qatar
11,437928,63569.4Doha
Uarabuni wa Saudia
1,960,58223,513,33012.0Riyad
Syria
185,18019,747,58692.6Dameski
Uturuki
756,76871,892,80776.5Ankara
Falme za Kiarabu
82,8804,621,39929.5Abu Dhabi
Yemeni
527,97023,013,37635.4Sana'a
Jumla43,810,5824,162,966,08689.07