Visasili vya Kigiriki

(Elekezwa kutoka Mitholojia ya Kigiriki)

Viasili vya Kigiriki ni jumla ya visasili vya Ugiriki ya Kale, yaani ukusanyaji wa masimulizi na hadithi kuhusu vyanzo, miungu na mashujaa wao. Ilikuwa moja ya sehemu za dini ya Ugiriki ya Kale.

Utatu wa Kigiriki na mgawanyo wa falme tatu za dunia: Zeus (mbingu), Poseidon (bahari) na Hade (kuzimu). Miungu midogo ni watoto wa watatu hao.
Kichwa cha Sanamu ya Zeu.

Chanzo kikuu kuhusu imani ya Wagiriki wa kale kabisa ni shairi la Theogonia lililotungwa na Hesiodo mnamo mwaka 700 KK.

Nasaba ya miungu ya Titani hariri

Titani aliyepinduliwa.

Watitani ni nasaba ya kwanza ya miungu katika visasili vya Kigiriki. Kiasili ni Watitani 12, wakiwemo 6 wa kiume na 6 wa kike wanaofunga ndoa kati yao na kuzaa Watitani wengine. Mkuu wao alikuwa Kronos hadi alipopinduliwa na mwanawe Zeus aliyeanzisha nasaba ya pili ya miungu ya Olimpos. Sehemu ya Watitani walijaribu kumpinga Zeus wakafukuzwa mbinguni.

  1. Hyperion – mungu wa nuru na jua, aliyemzaa mungu wa jua Helios, mungu wa kike wa mwezi Selene na mungu wa kike wa mapambazuko Eos
  2. Iapetosmume wa Klymene (binti wa Okeanos), aliyefukuzwa baadaye mbinguni
  3. Koios, aliyefukuzwa baadaye mbinguni
  4. Kreios – mume wa Eurybia
  5. Kronos – mkuu wa Watitani, baba wa Zeus, mume wa Rhea; alipinduliwa na Zeus akafukuzwa mbinguni akitawala kisiwa cha heri
  6. Mnemosyne – mama wa Muzi tisa
  7. Okeanos – mkuu wa bahari na himaya ya maji, baba wa miungu yote ya mito na pepo wa bahari na visima
  8. Phoibe – mke wa Koios, mungu wa mwezi
  9. Rheamama wa Hestia, Demeter, Hera, Hades, Poseidon na Zeus; alimfuata mumewe Kronos alipoondoka mbinguni
  10. Themis – mungu wa kike wa haki na mke wa pili wa Zeus; anajua wakati ujao
  11. Tethys – mke wa Okeanos
  12. Theia – mke wa Hyperion

Miungu Kumi na Miwili ya Olimpos hariri

Jina la KigirikiJina la KiswahiliMaelezo
Aφροδίτη (Afrodítē)AfroditaMungu wa kike wa upendo na uzuri.
Aπόλλων (Apóllōn)ApoloMungu wa nuru na ushairi.
Άρης (Árēs)AresMungu wa vita.
Άρτεμις (Ártemis)ArtemiMungu wa kike wa uwindo.
Αθηνά (Athēná)AthenaMungu wa kike wa elimu na hekima.
Δημήτηρ (Dēmḗtēr)

Δήμητρα (Dḗmētra)

DemetraMungu wa kike wa mimea na kilimo.
Διόνυσος (Diónysos)DionisoMungu wa divai.
Έρως (Érōs)EroMungu wa mapenzi.
ᾍδης (Ádēs)HadeMungu wa kuzimu na bwana wa waliokufa.
Ήφαιστος (Ḗfaistos)HefaistoMungu wa uhunzi.
Ήρα (Ḗra)HeraMungu wa kike wa ndoa na malkia ya miungu.
Ερμής (Ermḗs)HermeMjumbe wa miungu.
Ἑστία (Estía)HestiaMungu wa kike wa moto.
Ποσειδῶν (Poseidṓn)

Ποσειδώνας (Poseidṓnas)

PoseidoniMungu wa bahari.
Ζεύς (Zeús)

Δίας (Días)

ZeuMungu wa radi na mfalme wa miungu.

Protogenoi hariri

Jina la KigirikiJina la KiswahiliMaelezo
Αιθήρ (Aithḗr)AitheriMungu wa anga.
Ἀνάγκη (Anágkē)AnankaMungu wa kike wa kudra.
Έρεβος (Érevos)EreboMungu wa giza.
Γαία (Gaía)GayaMungu wa kike wa ardhi.
Ημέρα (Ēméra)HemeraMungu wa kike wa mchana.
Χάος (Kháos)Khaos
Χρόνος (Khrónos)KhronoMungu wa muda.
αἱ Nῆσοι (ai Nḗsoi)VisiwaMiungu ya kike wa visiwa.
Νύξ (Nýx)NiksiMungu wa kike wa usiku.
Ουρανός (Ouranós)UranoMungu wa mbingu.
Ούρος (Oúros)MilimaMiungu ya milima.
Πόντος (Póntos)PontoMungu wa bahari ya dunia nzima.
Τάρταρος (Tártaros)TartaroMungu wa tartaro.
Θάλασσα (Thálassa)ThalasaMalkia wa bahari na mke wa Ponto.

Titani Kumi na Wawili hariri

Jina la KigirikiJina la KiswahiliMaelezo
Ὑπερίων (Yperíōn)HiperioniMungu wa nuru ya jua.
Ἰαπετός (Iapetós)Yapeto
Κοῖος (Koïos)KoyoMungu wa fahamu.
Κρεῖος (Kreïos)Kreyo
Κρόνος (Krónos)KronoMfalme wa Titani.
Mνημοσύνη (Mnēmosýnē)MnemosinaMungu wa kike wa kumbukumbu.
Ὠκεανός (Ōkeanós)OkeanoMungu wa bahari kuu.
Φοίβη (Foívē)Foiba
Ῥέα (Réa)ReaMalkia wa Titani na mke wa Krono.
Τηθύς (Tēthýs)TethiMungu wa kike wa mito.
Θεία (Theía)TheyaMungu wa kike wa uonaji.
Θέμις (Thémis)Themi

Majitu hariri

  • Siklopsi (Κύκλωψ) - majitu-chongo watatu.
    • Arge (Ἄργης)
    • Bronte (Βρόντης)
    • Sterope (Στερόπης)
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
🔥 Top keywords: