Darubini ya anga-nje

Darubini ya angani (ing. Space observatory au space telescope) ni kifaa hasa darubini kilichorushwa katika anga la nje kwa kusudi la kuangalia na kupima violwa vya mbali kama vile nyota, sayari, galaksi na magimba mengine. Faida yake ni ya kwamba inaweza kuchungulia violwa hivi nje ya angahewa ya Dunia. Angahewa ni kama chujio inayozuia sehemu za spektra ya mawimbi ya sumakuumeme pia huwa na mwendo ndani yake unaoleta machafuko wa namna ya kuona nyota. Kwa hiyo darubini za angani zinaweza kuleta matokeo mazuri zaidi kushinda vifaa kwenye paoneaanga duniani.

Hubble ni moja ya darubini ya anga-nje mashuhuri

Darubini za angani kwa kawaida ziko kwenye obiti ya kuzunguka Dunia au zinawekwa kwa umbali ambako graviti ya Jua na Dunia inajisawazisha yaani kwenye nukta ya Lagrange. Darubini ya Spitzer inafuata obiti ya kuzunguka Jua.

Utazamaji wa nyota kutoka kifaa kilichopo angani unawezesha vipimo nje ya spektra za nuru inayoonekana na mawimbi ya redio kama vile mawimbi ya infraredi na urujuanimno ambayo yanazuiliwa na angahewa. Pia picha zinazochukuliwa nje ya angahewa ambako miale ya nuru hazipiti kwenye uchepuko wa tabaka za hewa ni bora kuliko picha zinazopigwa duniani.

Darubini za angani muhimu (si orodha kamili)

JinaTarehe ya kurushwaMwishoUpeo wa vipimoIsimamizi na
1968 / 19731977
Uhuru (SAS-1)19701973eksireiNASA
Orbiting Astronomical Observatory 3 (Copernicus)19721981urujuanimno, eksireiNASA
COS-B19751982gammaESA
International Ultraviolet Explorer19781996urujuanimnoNASA, ESA, SERC
Infrared Astronomical satellite19831983infraredi
Astron (satelaiti)19831989urujuanimno, eksireiUmoja wa Kisovyeti/Ufaransa
EXOSAT19831986eksireiESA
Ginga19871991eksireiISAS
Cosmic Background Explorer (COBE)19891993mikrowevuNASA
Hipparcos19891993nuru inayoonekanaESA
ROSAT19901999eksireiDLR
Hubble1990nuru inayoonekana, urujuanimno, infrarediNASA, ESA
Compton gamma Ray Observatory19912000gammaNASA
Yohkoh19912001eksireiISAS
Extreme Ultraviolet Explorer19922001urujuanimnoNASA
Advanced satelaitie for Cosmology and Astrophysics (ASTRO-D)19932000eksireiISAS
Infrared Space Observatory19951998infrarediESA
Solar and Heliospheric Observatory1995nuru inayoonekana, urujuanimnoNASA, ESA
Rossi X-ray Timing Explorer (RXTE)19952012eksireiNASA
BeppoSAX19962002eksireiASI
Far Ultraviolet Spectroscopic Explorer19992007urujuanimnoNASA
Chandra (darubini)1999eksireiNASA
XMM-Newton1999eksireiESA
Wilkinson Microwave Anisotropy Probe (WMAP)20012010mikrowevuNASA
Integral (satellite)2002gammaESA
Galaxy Evolution Explorer20032013urujuanimnoNASA
Spitzer darubini ya anga-nje2003infrarediNASA
MOST (satellite)2003CSA
Swift (satellite)2004gammaNASA
ASTRO-E (Suzaku)2005eksireiJAXA
ASTRO-F (Akari)20062011infrarediJAXA
COROT (darubini ya anga-nje)20062013nuru inayoonekanaCNES/ESA
AGILE2007gammaASI
Fermi gamma-ray Space Telescope2008gammaNASA
Kepler (darubini ya anga-nje)20092013nuru inayoonekana, infrarediNASA
Planck (darubini ya anga-nje)20092013mikrowevuESA
Herschel (darubini ya anga-nje)20092012 für HFIinfrarediESA
Wide-Field Infrared Survey Explorer20092011infrarediNASA
RadioAstron (Spektr R)2011mikrowevuIdara ya stronomia ya Taasisi ya Lebedew kwa Fizikia, Moskwa[1]
NuSTAR2012eksireiNASA
NEOSSat2013nuru inayoonekanaCSA
Gaia2013nuru inayoonekanaESA
ASTRO-H (Hitomi)2016eksireiJAXA, NASA, ESA, CSA
Hard X-ray Modulation Telescope (HXMT)2017eksireiCNSA
James Webb (darubini ya anga-nje)2021infrarediNASA, ESA, CSA
Public Telescope (PST)2019 (inapangwa)nuru inayoonekana, Ultraviolett (urujuanimno)astrofactum[2]
ASTRO-1 Telescope2020 (inapangwa)nuru inayoonekana, Ultraviolett (urujuanimno)BoldlyGo Institute[3][4]
Euclid (darubini ya anga-nje)2020 (inapangwa)nuru inayoonekana, nahes infrarediESA
  1. RadioAstron Archived 31 Desemba 2011 at the Wayback Machine., Lebedew-Institut für Physik, abgerufen am 30. August 2011.
  2. Ein privates darubini ya angani für Amateure und Profis
  3. "Astro-1 Space Telescope". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-11-26. Iliwekwa mnamo 2022-03-27.
  4. Corning Donates $1.8 Million in Parts for ASTRO-1 Telescope