Madini silikati

Madini silikati ni madini yanayounda miamba mbalimbali. Yote yanaundwa na anioni zenye silikoni na oksijeni. Ndilo kundi kubwa na muhimu zaidi katika madini yote likifanya karibu asilimia 90 za ganda la Dunia. [1] [2] [3]

Silika (dioksidi ya silikoni) SiO2 kawaida huhesabiwa kuwa madini silikati. Silika hupatikana katika maumbile kama shondo na maumbo yake.

Muundo wa msingi wa anioni ya SiO4. Mpira wa kijivu unawakilisha atomi ya silikoni, na mipira myekundu ni atomi za oksijeni.

Muundo wa jumla

hariri

Madini silikati kimsingi ni kampaundi ya ioni ilhali anioni zake huwa na atomi za silikoni na atomi za oksijeni.

Katika madini mengi kila atomi ya silikoni iko katikati ya kitovu cha piramidi pembetatu (tetrahedron), ambako pembe zake ni atomi za oksijeni nne.

Kikundi kikuuMuundoFomulaMfano
Nesosilikatipekee ya silicon tetrahedra[SiO 4 ] 4−olivine
Sorosilikatitetrahedra mara mbili[Si 2 O 7 ] 6−epidote, kikundi cha melilite
Saiklosilikatipete[Si n O 3 n ] 2 n -kikundi cha tourmaline
Inosilikatimnyororo mmoja[Si n O 3 n ] 2 n -kikundi cha pyroxene
Inosilikatimnyororo mara mbili[Si 4 n O 11 n ] 6 n -kikundi cha amphibole
Filosilikatishuka[Si 2 n O 5 n ] 2 n -mica na clay
TektosilikatiMfumo wa 3D[Al x Si y O (2 x +2 y ) ] x -shondo, feldspars, zeolites

Marejeo

hariri
  1. "Mineral - Silicates". britannica.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Oktoba 2017. Iliwekwa mnamo 8 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Deer, W.A.; Howie, R.A.; Zussman, J. (1992). An introduction to the rock-forming minerals (toleo la 2nd). London: Longman. ISBN 0-582-30094-0.
  3. Hurlbut, Cornelius S.; Klein, Cornelis (1985). Manual of Mineralogy (toleo la 20th). Wiley. ISBN 0-47180580-7.

Viungo vya nje

hariri
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Madini silikati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.