In My Own Words


In My Own Words ni albamu ya kwanza ya mwimbaji-mtunzi wa R&B Ne-Yo. Albamu ilitoka mnamo tar. 28 Februari 2006. Nyimbo nne zilipata kutolewa katika albamu hii, "Stay", "So Sick", "When You're Mad", na "Sexy Love".

In My Own Words
In My Own Words Cover
Kasha ya alabamu ya In My Own Words.
Studio album ya Ne-Yo
Imetolewa 28 Februari 2006 (2006-02-28)
Imerekodiwa 2005
Aina R&B, pop
Urefu 53:15
Lugha Kiingereza
Lebo Def Jam
Mtayarishaji Stargate, Shea Taylor, Ron Feemstar, Curtis Wilson
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za Ne-Yo
In My Own Words
(2006)
Because of You
(2007)
Single za kutoka katika albamu ya In My Own Words
  1. "Stay"
    Imetolewa: 2 Agosti 2005
  2. "So Sick"
    Imetolewa: 24 Januari 2006
  3. "When You're Mad"
    Imetolewa: 28 Februari 2006
  4. "Sexy Love"
    Imetolewa: Julai 2006

Wimbo wa kwanza kutolewa ulikuwa, "Stay", lakini hakumpa mafanikio makubwa na kuufanya kuwa wimbo pekee wa Ne-Yo, ambao haukupata kufikia chati za Billboard Hot 100 bora. Albamu ilipata kushika nafasi ya kwanza katika Billboard 200 kwa kuuza nakala zipatazo 301,000 katika wiki ya kwanza.

Badala ya hapo, kunako mwezi Agosti 2006, Ne-Yo akaanza kufanya matamasha na kuzunguka katika miji ya mbalimbali huku akiwa na baadhi ya wasanii wenzake kama vile Chris Brown na Dem Franchize Boyz. Baadaye albamu ikafikia kiwango cha platinam 1 kwa kuuza nakala mil. 1.6 kwa Marekani, na kopi milioni 2 kwa mauzo ya dunia nzima.

Maelezo

hariri

Ne-Yo ndiyo alioandika nyimbo za albamu nzima. Watayarishaji wa Kinorwei (Stargate) wametayarisha wimbo wa, "So Sick", na pia wamechangia mawili-matatu katika wimbo wa "Sexy Love", "Let Go", na "Time" kwa ajili ya LP ya kwanza.

Watayarishaji wengine katika albamu hii ni kama vile Ron "Neff-U" Feemstar, Brain "B-Nasty" Reed, na Jai "King" Titus of Drama Family Entertainment, ambaye ametayarisha wimbo wa kwanza, "Stay", na "Sign Me Up". "Let Me Get This Right" ni kazi nyingine ya wana Drama Family Entertainment.

Orodha ya nyimbo zilizopo

hariri
#JinaWatayarishajiMuda
1"Stay" (akimshirikisha Peedi Peedi)Drama Family Entertainment3:54
2"Let Me Get This Right"Drama Family Entertainment3:47
3"So Sick"Stargate3:27
4"When You're Mad"Shea Taylor3:43
5"It Just Ain't RightCurtis "Sauce" Wilson3:48
6"Mirror"Shea Taylor3:48
7"Sign Me Up"Drama Family Entertainment3:27
8"I Ain't Gotta Tell You"Boola3:17
9"Get Down Like That"Ervin "EP" Pope4:05
10"Sexy Love"Stargate3:40
11"Let Go"Stargate3:48
12"Time"Stargate3:29
13"Girlfriend" (UK bonus track)4:00
14"Get Down Like That (Remix)" (akimshirikisha Ghostface Killah) (UK bonus track)Urban "EP" Pope4:57

Chati

hariri
Chati (2006)Nafasi
Iliyoshika
Australian ARIA Albam na Chati za Mjini[1]41
Austrian Albums Chart63
Dutch Albums Chart[1]50
French Albums Chart[1]20
German Albums Chart27
New Zealand RIANZ Albums Chart35
Swiss Music Charts[1]11
UK Albums Chart[1]14
U.S. Billboard 2001
U.S. Billboard Top R&B/Hip-Hop Albums1

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Ne-Yo - In My Own Words - Music Charts αCharts. Accessed 20 Septemba 2008.

Viungo vya nje

hariri
🔥 Top keywords: