Bernardo wa Menthon

Bernardo wa Menthon, C.R.S.A. (au Bernardo wa Montjoux; Aosta, Italia, 1020 - Novara, Italia, 12 Juni 1081) alikuwa padri Mwaugustino mwanzilishi wa shirika la kitawa[1] ambalo lipo hadi leo likiwa na wanachama 40 wenye nadhiri.

Sanamu yake juu ya mlima Piccolo San Bernardo.
Mt. Bernardo katika bendera ya kikundi fulani.

Baada ya kuwa shemasi mkuu wa Aosta, aliishi miaka mingi katika vilele vya Alpi alipoanzisha monasteri na hosteli mbili za kupokelea wageni.

Tangu kale aliheshimiwa kama mtakatifu; hatimaye mwaka 1681 Papa Inosenti XI alithibitisha sifa hiyo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Juni[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.