Baikonur
Baikonur (kwa Kikazakhi: Baıqonyr / Байқоныр; kwa Kirusi: Байконур) ni jina la miji miwili nchini Kazakhstan.
- Baikonur ya kiasili ni mji mdogo kando ya mto Baikonur katika mkoa wa Karaganda uliokuwa na wakazi 427 kwenye mwaka 2009; kuna migodi ya makaa mawe.
- Baikonur unaojulikana kimataifa kama kituo cha kurushia vyombo vya anga-nje ni mji kwenye ukingo wa kaskazini wa mto Syr Darya. Umekodishwa na kutawaliwa na Shirikisho la Urusi.
Kituo cha kurushia roketi kilianzishwa mnamo mwaka 1955 karibu na kijiji cha Tyutaram wakati Kazakhstan ilipokuwa jamhuri ndani ya Umoja wa Kisovyeti; mwanzoni Umoja wa Kisovyeti ulijaribu kuficha mahali pake na baada ya mafanikio ya kwanza jina la "Baikonur" lilitangazwa hadharani kama mahali pa kurushia roketi. Mji ulikua hapa kwa makazi ya wanasayansi na wafanyakazi wa kituo. Ndani ya Umoja wa Kisovyeti walitumia pia jina la Звездоград (Zvezdograd) yaani "mji wa nyota"[1].
Tangu mwaka 1995, Urusi ilitumia rasmi jina la "Baikonur" kwa ajili ya mji huo.
Marejeo
hariri- ↑ Barensky, C.; Lardier, Stefan (2013). The Soyuz launch vehicle the two lives of an engineering triumph. New York: Springer. uk. 189. ISBN 978-1461454595.
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoLucy KombaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaSiku ya ArafahSiku ya Mtoto wa AfrikaKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoMikoa ya TanzaniaMaalum:MabadalikoyaKaribuniLuhaga Joelson MpinaKumaDiamond PlatnumzTanzaniaOrodha ya makabila ya TanzaniaKamusi za KiswahiliSimba S.C.Orodha ya Watakatifu WakristoNikki wa PiliKalenda ya KiislamuMaumivu ya kiunoMbooShairiNembo ya TanzaniaAmri KumiVita Kuu ya Pili ya DuniaTendo la ndoaIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Orodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaJohn MagufuliHistoria ya KanisaMofimuIdd el HajjOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaOrodha ya miji ya kale ya WaswahiliMapenzi ya jinsia mojaOrodha ya Marais wa TanzaniaFasihi simuliziOrodha ya Marais wa Zanzibar