Anthony Anderson

Anthony Alexandre Anderson (amezaliwa tar. 15 Agosti 1970) ni mwigizaji wa filamu, mchekeshaji, na mwandishi kutoka nchini Marekani. Amepata kucheza kwenye ucheshi wake mwenyewe wa All About the Andersons, vilevile kwenye igizo kama vile K-Ville, The Shield na Law & Order. Pia amepata kucheza kama mwigizaji mwandamizi kwenye filamu kama vile Transformers, The Departed, na Agent Cody Banks 2: Destination London.

Anthony Anderson

Anderson mnamo 2010, mjini Los Angeles
AmezaliwaAnthony Alexandre Anderson
15 Agosti 1970 (1970-08-15) (umri 53)
Los Angeles, California, U.S.
Kazi yakeMwigizaji
Miaka ya kazi1995–mpaka sasa
NdoaAlvina Anderson (1995-mpaka sasa)

Maisha ya awali hariri

Anderson alizaliwa mjini Los Angeles, California, akiwa kama mtoto wa Dora, mshughulikiaji simu na mwigizaji; baba yake wa kufikia, Sterling Bowman, ana miliki maduka mengi ya nguo.[1] Anderson ni mhitimu wa Los Angeles County High School for the Arts na [[Chuo Kikuu cha Howard. Amesoma na waigizaji wenzake kama vile Avery Brooks, Ruby Dee na Ossie Davis.[2]

Shughuli hariri

Anderson amekuwa akifanya kazi kama mwigizaji, hasa kwenye nyanja za uchekeshaji, kwa miaka mingi. Kazi zake za televisheni ni pamoja na kuonekana san akiwa kama nyota mwalikwa kwenye mfululizo wa NYPD Blue, Malcolm & Eddie, In the House, na Ally McBeal. Nyusika zake zilizokuwa zikijirudia ni pamoja na mfululizo wa Til Death na The Bernie Mac Show. Alikuwa muhusika wa kati kwenye mfululizo wa All About the Andersons, ambao uliishia kwa msimu mmoja tu kwenye televisheni ya the WB.

Miongoni mwa suhirika wake maarufu ni pamoja na filamu ya: Kangaroo Jack, My Baby's Daddy, Hustle & Flow, na Agent Cody Banks 2: Destination London.

Anderson amejiunga kwenye igizo refu la TV la uharifu la NBC, Law & Order mnamo 2008. Awali alipata kuonekana kwenye mifululizo mingine miwili ya uharifu, K-ville (akiwa kama mmoja kati ya wahusika wakuu) na The Shield.

Kazi za uongozaji hariri

Mnamo mwaka wa 2009, Anderson amepata kuongoza filamu-fupi ya dakika moja akishirikiana na nyota mwenzi wa kwenye Law & Order,Jeremy Sisto. Filamu hiyo ilitengenezwa kwa ajili ya Responsibility Project, mpango unganishi wa NBC na Liberty Mutual Group. Kipande hicho kilirushwa wakati wa onyesho la Law & Order katika kipengele cha "Reality Bites" mnamo tar. 16 Oktoba 2009.

Maisha binafsi hariri

Mnamo mwaka wa 1995, amemwoa kipenzi chake cha roho waliokuwa wakisoma wote chuo Bi. Alvina. Wawili hao wana watoto wawili. Kwa sasa wanaishi mjini Hancock Park, Los Angeles, California.

Filmografia hariri

MwakaFilamuKama
1999Liberty HeightsScribbles
LifeCookie
Trippin'Z-Boy
2000Romeo Must DieMaurice
Big Momma's HouseNolan
Me, Myself & IreneJamaal Baileygates
Urban Legends: Final CutStan Washington
2001See Spot RunBenny
Exit WoundsT.K. Johnson
Kingdom ComeJunior Slocumb
Two Can Play That GameTony
3 StrikesAskari
2002BarbershopJ.D.
2003Kangaroo JackLouis Booker
Cradle 2 the GraveTommy
Malibu's Most WantedPJ
Scary Movie 3Mahalik
2004My Baby's DaddyG. Bong
Agent Cody Banks 2: Destination LondonDerek Bowman
Harold & Kumar Go to White CastleBurger Shack Employee
2005The Bernie Mac ShowBryan Brown
King's RansomMalcolm King
Hustle & FlowKey
Hoodwinked!Detective Bill Stork
Alone in the DarkPhoto of missing person
2006Scary Movie 4Mahalik
The Last StandJay
Arthur & the InvisiblesKoolomassai
The DepartedTrooper Brown
2007TransformersGlen Whitmann
2010The Back-Up PlanDad
2011Scream 4Detective Perkins
The Big YearBill Clemens
2013Scary Movie 5Mahalik

Tamthiliya hariri

MwakaTamthiliyaKama
1996–1998Hang TimeTeddy Broadis
2001 My Wife and KidsMarriage Counsellor, Dr. Buchay
2003–2004All About the Andersons-
2004–2005The ShieldAntwon Mitchell
2006Law & Order: Special Victims UnitLucius Blaine
2007K-VilleMarlin Boulet
2008–2010Law & OrderDetective Kevin Bernard
2008Samantha WhoRafael Grace
2010–hadi leoGolf in AmericaHost[3]
2012PsychChef Thane Woodson
2012The Soul ManSweet Brown Taylor
2012-2013Guys with KidsGary
2010-2013TremeDerek Watson
2013Hollywood Game NightMwenyewe
2014RakeReggie Jarvis
2014-hadi leoBlackishAndre "Dre" Johnson, Sr.

Marejeo hariri

  1. Anthony Anderson Biography (1970-)
  2. Comic in 'K-Ville' - Los Angeles Times
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-02-24. Iliwekwa mnamo 2012-08-23.

Viungo vya Nje hariri