Antonio Gonzalez (mfiadini)

Antonio Gonzalez, O.P. (takriban 1593 - 24 Septemba, 1637) ni mmojawapo kati ya Wakristo waliofia dini nchini Japani kwa amri ya Shogun Tokugawa Yemitsu (1633-1637).

Mchoro wa Kijapani ukiwaonyesha Wafiadini wa Nagasaki, karne ya 16 na ya 17.

Alikwenda huko kama padri mmisionari kutoka Hispania, akitokea Ufilipino pamoja na wenzake 5.

Alifariki gerezani kutokana na mateso ya kikatili aliyoyapata [1].

Anaheshimiwa kama mtakatifu pamoja na Lorenzo Ruiz na wenzao waliotangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa wenye heri tarehe 18 Februari 1981 halafu watakatifu tarehe 18 Oktoba 1987.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Lorenzo de Manila, The Proto-Martyr of The Philippines and his Companions - Fr. Fidel Villarroel, O.P., 1988
  • Constantino Alvares, Jose Garcia, Pedro Tejero, Witnesses of the faith in the Orient: Dominican Martyrs of Japan, China, and Vietnam, Manila, Life Today Publications, 1989, ISBN 971-8596-03-8
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.